na wao wenyewe wanaweza kuamua aina ya kilimo au aina ya mazao
watakayopenda kupanda kwenye majaribio yao. Wanaweza kuchagua kupanda
mahindi au mazao mengine kama jamii ya maharage. Sehemu moja isiwekwe
mbolea yoyote na maeneo mengine yanaweza kuwekwa mboji, mbolea za
mimea iliyooza na mbole zinazoatoka mazizini. Wakulima wanaweza vilevile
kuweka mbolea za viwandani ambazo zina mchanganyiko wa fosforasi mfano
mbolea ya triple super phosphate (TSP) au rock phosphate (PR) ili kuona tofauti
kati ya mbolea za viwandani na mbole za asili kama chanzo cha fosforasi katika
ukuzaji wa mimea.
Hakuna sheria maalum za kufuata, jambo la msingi ni kuongeza mazoezi au
uzoefu wa majaribio kwa wakulima na kuimarisha uelewa wao kuhusu umuhimu
wa fosforasi kwa mimea. Zoezi hili pia hujenga uwezo wa wakulima (ujuzi, kuwa
katika vikundi na kushirikiana) katika kuanzisha majaribio yao wenyewe. Hatua
muhimu za kufuta wakati wa kuanzisha jaribio ni kama ifuatavyo:
➢ Kuangalia uzoefu wa wakulima kwa vipindi vya nyuma (ni majaribio gani
walikwisha fanya kabla? Walifanyaje? Kwanini walifanya hivyo, je
walifanikiwa?
➢ Kubuni na kupanga majaribio na wakulima (ni wakina nani hasa watahusika
na kufanya majaribio? Je kuwepo na majaribio ya kuweza kutumika kama
vielelezo (controls)? Je ni maeneo yapi yatakuwa muafaka kwa majariobio?
Ni maeneo kiasi gani yanahitajika? Ni vitu gani vinahitajika kutumika? Jaribio
litapangwa vipi? Ni vitu gani vinahitajika na vitapatikanaje?
➢ Kuweka utaratibu wa kutathmini majaribio (ni vigezo gani vitumike katika
kutathmini yaliyotokea kwenye majaribio? Nini na ni lini itahitajika kuangalia,
kupima kujadili na kuweka kumbukumbu na haya yote yatafanyikaje? Ni nani
atahusika?
➢ Wakulima watangaziwe. Pengine wengine watapenda kushirikiana na
wakulima wengine katika kupima mafanikio yao. Mafunzo ya mkulima kwa
mkulima ni nafasi au muda muafaka kwa ajili ya kuwashirikisha wakulima
kwenye majadiliano na kubadilishana uzoefu. Kuwaalika wakulima toka
makundi mengine kutembelea mashamba ya majaribio ni jambo lingine katika
kubadilishana matokeo ya majaribio na kuwafundisha wengine umuhimu wa
fosiforasi kwa ukuaji wa mazao.
Muhimu ni vikundi vya wakulima kukutana mara kwa mara katika maeneo
ambapo majaribio yapo kwa kufuatilia na kutathmini majaribio.
Kutoka kwa Bashir Jama, muunganishaji wa Afrika mashariki na kati katika
ICRAF,
kuhusu maonyesho katika mashamba.
Magharibi mwa Kenya, mna ploti ndogo ndogo zinazotumika kudhbitisha
upungufu wa madini. Hizo ploti huwa 3x3m na huwa na:
17